watu takribani 80 wameripotiwa kufariki dunia na makumi wengine kujeruhiwa katika msongamano na kukanyagana wakisherekea sikukuu ya Eid katika tamasha la muziki lililofanyika katika mji mkuu wa Guinea Conakry. Tukio hilo limetokea katika eneo la Ratoma ambapo kundi maharufu la muziki wa rap "Instinct Killers" la nchini humo na wasanii wengine walikuwa wakifanya tamasha la sikukuu ya Eid al Fitri kusherekea kukamilisha mfungo wa Ramadhani. maaafa haya yametokea wakati nchi ya Guinea ikikabiliwa na janga la ugonjwa wa Ebola unaozidi kuenea kwa kasi katika nchi za Afrika Magharibi. Ofisi ya Raisi wa Guinea Conakry imetangaza wiki nzima ya maombolezo ya kitaifa ya maafa hayo. Vyombo vya usalama vya Guinea vimeanza uchunguzi kubaini mazingira na chanzo cha maafa hayo. Habari kwa hisani ya Iran Swahili Radio
Leave a Comment