Ray c Foundation yazidi kupaa,Project yake ya SHULE KWA SHULE tayari ishahudumia zaidi ya shule 30, RAY C afunguka asema anatamani kutanua huduma zake ila fedha ni changamoto kubwa inayomkwamisha.,
Ray C foundation taasisi iliyoanzishwa na msanii wa Bongo Flava Rehema Chalamila Ray C kwa ajili ya kusaidia vijana walioathirika kwa madawa ya kulevya na kutoa elimu juu ya athari za madawa hayo,imezidi kupata mafanikio na kuzidi kupaa baada ya mradi wake wa SHULE KWA SHULE CAMPAIGN,kuzifikia zaidi ya shule 30 jijini Daressalaam.
Mradi wa SHULE KWA SHULE umelenga kuelimisha wanafunzi wa shule kuhusu athari za madawa ya kulevya ili kuwaokoa wanafunzi walioanza kutumia pia kuwaepusha wengine kuanza kutumia dawa hizo.
Akiongea na mtangazaji wa kituo cha Saut fm 96.1mhz cha jijini Mwanza,Ray C amesema kuwa anatamani shughuli za tasisi hiyo zifikie mikoa mingine Tanzania lakini Fedha imekuwa changamoto kubwa kwake.
"Ningependa wafadhili wajitokeze kwa wingi,serikali pia inisaidie ili niweze kuwafikia walengwa wengi zaidi manake waathirika wa madawa ya kulevya wako mikoa yote sio Daressalam peke yake" aliongeza Ray C ambaye pia aliwahi kunusurika kifo baada ya kuathirika kwa matumizi ya madawa ya kulevya kabla ya kupata matibabu.
Click hapa kusikiliza sauti ya RaY C akizungumza
Mradi wa SHULE KWA SHULE umelenga kuelimisha wanafunzi wa shule kuhusu athari za madawa ya kulevya ili kuwaokoa wanafunzi walioanza kutumia pia kuwaepusha wengine kuanza kutumia dawa hizo.
![]() |
Ray C akimshukuru raisi Kikwete kwa kumwezesha kupata matibabu baada ya kuathirika na madawa ya kulevya |
"Ningependa wafadhili wajitokeze kwa wingi,serikali pia inisaidie ili niweze kuwafikia walengwa wengi zaidi manake waathirika wa madawa ya kulevya wako mikoa yote sio Daressalam peke yake" aliongeza Ray C ambaye pia aliwahi kunusurika kifo baada ya kuathirika kwa matumizi ya madawa ya kulevya kabla ya kupata matibabu.
Click hapa kusikiliza sauti ya RaY C akizungumza
Leave a Comment