Facebook na Apple kugandisha mayai ya uzazi kwa wafanyakazi wake wa kike hadi watapokuwa tayari kushika mimba
Wanawake wanaofanya kazi na kampuni za Facebook na Apple wanapewa nafasi ya kipekee katika kazi yao,Wanapewa fursa ya kugandisha Mayai yao ya uzazi hadi watakapokuwa tayari kushika mimba.
Facebook tayari ilishanza kutoa huduma hii kwa wafanyakazi wake wanawake nchini Marekani tangu mwanzoni mwa mwaka huu.Sera hii inalenga kuwavutia wanawake kufanya kazi na Facebook na pia kwa Facebook kupata wafanyakazi wazuri wenye kipaji na kuwasaidia kuchagua kati ya kazi na uzazi.
Nayo kampuni ya Apple inajiandaa kuanzisha sera hii ifikapo Januari mwaka 2015.
"tunaendelea kuwapa faida nyingi wanawake , kwa kuwaongeza muda wa kupumzika baada ya kujifungua, pamoja na kuhifadhi mayai yao kama sehemu ya mpango wa kuwasaidia baadaye ikiwa watakosa kushika mimba, '' ilisema taarifa ya kampuni ya Apple.
Kampuni hizo mbili, zinatoa hadi dola elfu 20 kwa wafanyakazi wanawake kuhifadhi mayai yao na kuyangadisha wakitarajia kuyatumia wakati watakapokuwa tayari kuzaa au ikiwa watapwa na tatizo la kushika mimba basi wataweza kuyatumia.Kuna ushindani mkubwa sana katika kuwaajiri wafanyakazi wenye talanta na kipawa pamoja na tajriba ya kazi na kampuni hizi pia zinataka kupata wafanyakazi bora wenye uzoefu wa kazi na watakaofanya kazi na kampuni hizo kwa mda mrefu.
Baadhi ya wadadisi wanasema jambo la kuhifadhi Mayai ya wanawake, linawapa uwezo zaidi wa kudhibiti kizazi hata hivyo kampuni hizi zinapaswa kuwa tayari kuwasaidia wanawake wanaoamua kupata watoto wakiwa wanafanya kazi badala ya kufanya jambo hili.
Tayari sera hii imekosolewa baadhi ya wanwake wakisema kampuni hizi zinajali zaidi faida badala ya kuabadilisha mazingira ya kazi na kufanya mambo kuwa mepesi kwa wanawake wanaofanya kazi nao.Kwa kuwa wanawake wengine huwa hawako tayari kushika mimba, kwa sababu labda ya maujukumu ya kikazi na kazi nyingi, wao hauamua kuhifadhi mayao ya o kwa mnjia ya kisayansi na kuyatumia baadaye watakapokuwa tayari.
Leave a Comment