MKURUGENZI WA KAMPUNI YA MUZIKI APIGWA RISASI

SUGE KNIGHT APIGWA RISASI
Mkurugenzi wa zamani wa kampuni ya muziki ya Deathrow ya Marekani, Suge Knight anaripotiwa kufanyiwa upasuaji hospitali kufuatia kupigwa risasi katika sherehe isiyo rasmi ya tuzo za video bora za MTV. Suge Knight inadaiwa alipigwa risasi kadhaa mapema siku ya Jumapili (Agosti 24), akiwa West Hollywood nightspot 1 Oak. Knight aliweza kuondoka huku akitembea mwenyewe katika sherehe hiyo iliyoandaliwa na Chris Brown, kabla ya polisi kumsaidia, kwa mujibu wa tovuti ya TMZ
Kwa hisani ukurasa wa facebook wa SALIM KIKEKE


No comments

julianDamas 2011 - 2014. Powered by Blogger.