(EXCLUSIVE) KUMBE JAGUAR ALIDANGANYA KUHUSU KUMILIKI NDEGE BINAFSI (PRIVATE JET)!!!
Wahenga walisema kuwa "njia ya mwongo ni fupi",na kwenye ukweli uongo hujitenga pembeni.
Nasema hivi kutokana kukua kwa tabia iliyoibuka miongoni mwa wasanii maharufu kudanganya umma kuhusu kumiliki mali za thamani,kutokuwa wazazi kumbe wapo hai vijijini au kudanganya kuhusu gharama za video na mambo mengine kadha wa kadha.
Achana na hayo hapa nataka nikujuze hili
Baada ya Video ya wimbo "KIPEPEO" wa msanii wa muziki wa kizazi kipya toka kenya JAGUAR kuonekana kila mtu aliamini JAGUAR anamiliki ndege iliyonekana katika video hiyo na hata JAGUAR mwenyewe alipoulizwa kuthibitisha ukweli kuhusu hilo alijibu "MUNGU AMENIBARIKI" na kuwaacha watu wapigie mstari kuwa ndege hiyo ni mali yake.
Sasa imefahamika kuwa ndege hiyo si mali yake bali ni ya Tajiri(Tycoon) kijana mwenye umri wa miaka 26 ambaye ni rafiki wa karibu wa msanii huyo anayemiliki kampuni ya usafirishaji inayoitwa BUSH AIR SAFARIS.
Inasemekana kuwa tajiri huyo alimwazima JAGUAR ndege hiyo kwa ajili ya kufanyia video ya wimbo huo na hata ukiitazama video hiyo kwa makini utaona logo(nembo) ya Bush Air Safaris kampuni inayomilikiwa na kijana huyo tajiri.
Itazame video hiyo hapa..
habari kwa hisani ya liz njuguna wa ghettoradio.co.ke na Ghetto radio fm kenya

Leave a Comment