UTATA: Alichoandika Lady Jaydee Instagram kuhusu picha ya Matonya akiwa amelala hoi vichakani
Katika hali ya sintofahamu mwanadada nguli wa muziki Tanzania Judith Wambura ( Lady Jaydee ), ame post picha ya mwanamuziki mwenzake Matonya iliyoonesha Matonya akiwa amelala hoi vichakani katika mtandao wa picha wa Instagram, huku ikiwa maandishi yenye ujumbe mzito ulioacha mashabiki wake na maswali Je Jaydee yuko serious au ni masihara / utani?.
Picha hiyo ya matonya ilianza kusambaa mitandao tokea siku ya jumanne tarehe 6 jan 2015 na kuzua maswali mengi kwa mashabiki wake je mkali huyo wa ngoma kama vaileth, anitha na zilipenda amekutwa na maswahibu gani? , Huku wengine wakisema ni picha za video mpya ya mkali huyo ( Tonya Time ) anaewakilisha vyema mkoa wa Tanga ki Bongo Fleva.
Ikumbukwe kuwa Matonya na LadyJaydee waliwahi kushirikiana katika wimbo uliowahi fanya vizuri Africa Mashariki " ANITHA " na hivi karibuni hakujawahi kusikika hadharani kuwa kuna tofauti kati ya wasanii hao wawili.Japo mwaka 2013 matonya alituhumiwa kupiga mkwanja kisha kutotokea kwenye show ya Lady Jaydee.
JE UNAHISI ALICHOKIANDIKA JAYDEE NI MASIHARA AU YUKO SERIOUS?
Tupia comment yako hapa
Leave a Comment