KINACHOJIRI: MAPINDUZI NCHINI UTURUKI
Rais wa
Uturuki Erdogan ajitokeza Istanbul
·
Kundi la wanajeshi lilitangaza
mapinduzi kupitia runinga ya taifa
Rais wa Uturuki Recep Tayyip
Erdogan amejitokeza katika uwanja wa ndege wa Istanbul, akiwa amezingirwa na
mamia ya wafuasi baada ya kundi la wanajeshi kujaribu kupindua serikali yake.
Kwenye kikao
cha dharura na wanahabari, ameahidi kusafisha jeshi na akaahidi kwamba wote
waliohusika wataadhibiwa vikali.
Kundi la
wanajeshi lilikuwa limetekeleza jaribio la kupindua serikali.
Taarifa kutoka
kwa kundi hilo la jeshi, ambayo ilisomwa kupitia runinga ya taifa ilisema jeshi
lilikuwa limechukua mamlaka.
Hata hivyo,
Waziri Mkuu wa Uturuki Binali Yildirim ameambia runinga moja ya Uturuki kwamba
hali imethibitiwa na kwamba waliohusika wataadhibiwa vikali.
Mashirika ya
haabri ya serikali yanaripoti kuwa majengo ya bunge mjini Ankara yamekumbwa na
mlipuko wa bomu.
Kituo cha
runinga cha kibinafsi cha NTV kinasema ndege ya kivita ya wanajeshi watiifu kwa
serikali imeidungua helikopta iliyokuwa ikitumiwa na wanajeshi waliotekeleza
jaribio la mapinduzi mjini Ankara.
Milio ya risasi
inasikika katika moja ya madaraja makubwa zaidi kwenye mto Bosphorus, katika
mji mkubwa zaidi Uturuki, Istanbul. Makabiliano yanadaiwa kuwa kati ya
wanajeshi na waandamanaji.
U
TERS
Wakati wa
kutangaza mapinduzi ya serikali, kundi hilo la wanajeshi lilisema lilichukua
hatua hiyo kuhifadhi utawala wa demokrasia na likatangaza amri ya kutotoka nje.
Lilisema nchi
hiyo ingeongozwa na “baraza la amani” ambalo lingehakikisha utulivu na usalama.
Aidha,
liliahidi kwamba utawala wa kikatiba ungerejeshwa “haraka iwezekanavyo”.
Jaribio hilo la mapinduzi ya serikali lilitekelezwa Rais Erdogan akiwa likizoni.
Alihojiwa baadaye kwenye runinga, kupitia simu na mtandao wa Facetime, ambapo alitoa wito kwa watu kujitokeza barabarani kuunga mkono demokrasia.
Raisi wa Uturukiakiongea na kituo cha CNN _ Turkey kwa njia ya mtandao |
Raisi Erdogan Alisema jaribio hilo la mapinduzi lilitekelezwa na kundi la wachache jeshini.
Marekani,
Urusi, NATO na Umoja wa Ulaya wote wamehimiza kuwepo kwa utulivu na uthabiti.
Waziri wa mambo
ya nje ya Marekani John Kerry amesisitiza kwamba Marekani itaunga mkono
serikali ya Uturuki iliyochaguliwa kidemokrasia pamoja na taasisi zake.
Habari kwa Mujibu wa
mtandao wa BBC Swahili
Leave a Comment